Utata wa Chanjo ya HPV 2019

Daktari Wahome: chanjo ya HPV si muhimu, hatuihitaji hata kidogo. Kulingana na Daktari Wahome Ngare, chanjo ya HPV ina madhara kama kupooza na hata pia kukomesha uwezo wa kupata ujauzito ilhali mapema, akidai ya kwamba, wazazi wameenda kortini huko maeneo ya Japan, Australia na India wakililia madhara hayo hayo yanayosababishwa na chanjo hiyo. Si hayo tu bali mwanzoni wa wiki iliyopita tarehe 21 mwaka 2019 mwenzi wa oktoba imesemekana ya kwamba, makanisa ya katholiki pamoja na maimamu wamekuwa na shauku juu ya usalama wa chanjo hiyo. Daktari Wahome pia aliuliza hivii, sisi kama wananchi tuko na uhakika gani kwamba hiyo chanjo ya HPV itasaidia kukinga cancer ya kizazi? Huku akinukuu ya kwamba chanjo ya HPV yakinga HPV ambayo ni magonjwa ya zinaa kwa ujumla. Alisisitiza ya kwamba, ili kuwa sahihi kuhusu chanjo ya HPV basi inatakiwa kuwe na wanawake wawili, mmoja ambae tayari ameambukizwa na virusi hvyo vya HPV na mwengine ambae hana virusi hivyo na kuwapatia hiyo chanjo na kusubiria matokeo yake huku wakifuatilia maisha yao. Hapo ndipo kutakuwa na uwazi kama chanjo hyo inakinga cancer ya kizazi au La! Lakini kama sote tunavyojua chanjo ya HPV ilianzishwa mwaka 2006 na kwa sasa tuko mwaka 2019, ndani ya hiyo miaka 13  Daktari Wahome anaamini kwamba, huo muda ni kidogo sana kujua uhalisi wa chanjo ya HPV. Chanjo ya HPV ikona madhara mengine kama kuumwa na kichwa au kuhisi uchovu, maumivu, wekundu au uvimbe katika mkono ambao ulidungwa sindano, homa, kichefuchefu na maumivu ya misuli au maumivu ya mwili mzima. Je? Chanjo ya HPV ni Baraka au ni laana. Hili ni jambo linalowahusisha watoto wote wa kike, si Kenya tu, Bali dunia nzima kwa ujumla. Source ; https://citizentv.co.ke/videos/?video=4NtbgPiWE3g Follow us on Twitter: https://twitter.com/mtotonews Subscribe to our YouTube Channel: http://youtube.com/mtotonewstv Mtoto News is a Digital Online platform of news, information and resources that aims at making significant change in the lives of children by making them visible. Read mtotonews.com or follow us on twitter and Facebook @mtotonewsblog     

0 Comment